UN yafanya mkutano kuijadili Taliban bila uwepo wa wao
1 Mei 2023Mkutano huo utahudhuriwa na Marekani, China na Urusi pamoja na wafadhali wakubwa wa misaada kutoka Ulaya na hata majirani muhimu wa Afghanistan kama Pakistan ni miongoni mwa nchi zitakazokuwa na wawakilishi kutoka karibu nchi na makundi 25.
Mkutano huo wa siku mbili utaongozwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres. Serikali ya Taliban haikualikwa jambo lililozua maswali kuhusiana na kutambuliwa kwa serikali hiyo.
Guterres, wajumbe kujadili mzozo wa Afghanistan
Kundi dogo la wanawake raia wa Afghanistan waliandamana mwishoni mwa wiki mjini Kabul kupinga hatua yoyote ya kuwatambua watawala hao waliorudi madarakani mnamo Agosti mwaka 2021.
Umoja wa Mataifa na Marekani wamesisitiza kwamba kutambuliwa kwa Taliban hakutokuwa kwenye ajenda ya mambo yatakayojadiliwa kwenye mkutano huo.