UN: Kutoa dola milioni 100 kuzisaidia nchi zenye migogoro.
20 Februari 2024Ufadhili huo utakaotolewa kutoka Mfuko wa hazina wa dharura wa Umoja wa Mataifa (CERF), ni mdogo zaidi kuwahi kutolewa katika miaka ya hivi karibuni, hasa ikizingatiwa kuwa mashirika ya misaada yanataabika kupata michango zaidi huku kukiwa na msururu wa majanga ya kibinadamu duniani.
Kulingana na Shirika la kiutu la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya dharura OCHA, mwaka jana, mahitaji ya misaada ya kimataifa yalifikia kiwango cha juu cha karibu dola bilioni 57, wakati migogoro ikiongezeka kama ule kati ya Israel na Hamas.
Wakaazi mashariki mwa Congo wakabiliwa na uhaba wa chakula
Mwezi uliopita shirika hilo lilisema uhitaji wa fedha na rasilimali nyengine ulifikia kiwango kisichotarajiwa cha dola kufuatia ahadi nyngi za fedha anbazo hazijatimizwa.