JamiiNiger
Umoja wa Mataifa kusitisha safari za kibinadamu Niger
30 Desemba 2023Matangazo
Hayo ni kutokana na ukosefu wa fedha huku jumla ya watu milioni 4.3 wakiwa wanahitaji msaada.
Katikati ya mwezi Novemba, shirika hilo la kimataifa lilitangaza kuanzisha tena safari zake katika nchi hiyo iliyokumbwa na mapinduzi ya kijeshi mnamo Julai 26 mwaka huu (2023), yaliyomuondoa madarakani rais aliyechaguliwa kidemokrasia, Mohamed Bazoum.
Mwakilishi na mkurugenzi wa WFP nchini Niger , Jean-Noel Gentile, amesema hali ya kifedha ya shirika la misaada la UNHAS tayari imeilazimisha kupunguza meli na ndege moja za kusafirisha misaada.
Mashirika mbalimbali ya misaada ya kimataifa kama WFP, UNHAS na OCHA wameelezea wasiwasi huo katika taarifa yao ya pamoja kutokana na ukosefu wa fedha na kutokuwa uhakika wa kupata ufadhili zaidi.