SiasaHaiti
Umoja wa Mataaifa waonya juu ya hali mbaya nchini Haiti
18 Machi 2024Matangazo
Mkuu huyo wa UNICEF, Catherine Russell amesema Haiti ime kwenye hali ya kutisha ambayo haijashuhudiwa katika miongo kadhaa.
Bi Russell amesema watu wengi wamekumbwa na njaa na utapiamlo na kwamba Umoja wa Mataifa unashindwa kufikisha msaada wa watu wa Haiti, kutokana na magenge kukidhibiti sehemu kubwa za mji mkuu wa Port-au-Prince pamoja na barabara kuu zinazoelekea kwenye miji mingine.
Ripoti ya hivi majuzi ya Umoja wa Mataifa imesema kutokana na kuwepo serikali dhaifu nchini Haiti, huduma za kimsingi zinakaribia kuporomoka nchini humo. Nchi hiyo pia inakumbwa na ukame na majanga ya asili.