1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Falme za Kiarabu kujenga uwanja wa ndege Uganda

21 Juni 2024

Uganda imetia saini mkataba na shirika la kibiashara kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kwa ajili ya ujenzi wa uwanja mpya wa ndege wa kimataifa.

https://p.dw.com/p/4hMvG
 Yoweri Museveni
Rais Yoweri Museveni wa Uganda.Picha: Darko Vojinovic/AP Photo/picture alliance

Hayo yameelezwa hivi leo na Ofisi ya Rais Yoweri Museveni.

Mwenyekiti wa Chama cha Biashara na Viwanda cha UAE chenye makaazi yake huko Sharjah, Abdallah Sultan Al-Owais, amesema wataanza ujenzi huo mwezi Agosti nje kidogo ya Hifadhi ya Kidepo kaskazini mashariki karibu na mpaka wa Uganda na Kenya.

Soma zaidi: Uganda yakanusha vikali kuwaunga mkono waasi wa M23

Mkataba huu wa ujenzi wa uwanja wa tatu wa ndege katika taifa hilo la Afrika Mashariki, unadhihirisha matarajio ya UAE kutanua nguvu zake za kiuchumi mbali na sekta za mafuta, gesi na nishati mbadala.