1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Afrika wazingatia ombi kuhusu wanajeshi Somalia

21 Juni 2024

Umoja wa Afrika umesema unalichunguza ombi la Somalia la kupunguza kasi ya kuondoka kwa vikosi vya kulinda amani vya umoja huo (ATMIS) vyenye jukumu la kupambana na kundi al-Shabaab lenye mafungamano na al-Qaida.

https://p.dw.com/p/4hLtr

Baada ya kikao kilichofanyika siku ya Alkhamis (Juni 20) mjini Addis Ababa, Ethiopia, mmoja wa wanadiplomasia wa Umoja wa Afrika alisema huenda baraza lake la amani na usalama likaridhia ombi la Somalia na kuchelewesha kwa miezi kadhaa mchakato wa kuondoka kwa vikosi vya ATMIS.

Soma zaidi: Somalia yataka mchakato wa kuondoka vikosi vya ATMIS ucheleweshwe

Maazimio ya Umoja wa Mataifa yamevitaka vikosi vya Tume ya Amani ya Umoja wa Afrika viondoke kwa awamu hadi kufikia Desemba 31 mwaka huu, na kukabidhi majukumu ya usalama kwa jeshi na polisi wa Somalia. 

Awamu ya tatu na ya mwisho ilitarajiwa kushuhudia wanajeshi 4,000 wakiondoka kufikia mwisho wa mwezi huu wa Juni.

Kufikia sasa wanajeshi 13,500 wa ATMIS wanahudumu nchini Somalia.