SiasaVenezuela
Umeme wakatika kote nchini Venezuela
31 Agosti 2024Matangazo
Kukatika kwa umeme kumeathiri pakubwa shughuli za kijamii katika taifa ambalo linakabiliwa na mzozo wa kisiasa tangu uchaguzi wa Julai 28.
Waziri wa Mawasiliano Freddy Nanez amelielezea tukio hilo kuwa ni hujuma, uhalifu na jaribio la mapinduzi ya kijeshi, mwezi mmoja baada ya uchaguzi wenye utata uliompa ushindi rais Nicolas Maduro.
Umeme ulikuwa ukirejea na kukatika tena katika baadhi ya maeneo ya Caracas na katika majimbo ya kusini-magharibi ya Tachira na Merida. Serikali hata hivyo imeahidi kurekebisha hali hiyo haraka iwezekanavyo.
Mara kadhaa mamlaka nchini humo zimekuwa zikisema kuwa vitendo vya hujuma huendeshwa na Marekani kwa ushirikiano na upinzani ili kuipindua serikali.