Ulaya na Marekani zasusia kutoa heshima kwa Raisi
31 Mei 2024Kikao hicho cha kutoa heshima ni utaratibu wa muda mrefu ambapo Baraza hilo la Umoja wa Mataifa lenye wanachama 193 hufanya mkutano maalumu kwa heshima ya kumbukumbu ya mkuu wa nchi mwanachama anapofariki.
Soma pia:Rais Assad wa Syria akutana na kiongozi Mkuu wa Iran Khamenei
Makundi yote ya kikanda ya Umoja wa Mataifa hutuma wawakilishi kuzungumza juu ya maisha ya mwendazake na urithi alioacha.
Rais Raisi alikumbukwa kwa sifa kemkem hasa kutoka mataifa ya Afrika.
Soma pia:Mamilioni ya waombolezaji wajitokeza kutoa heshima zao kwa Rais Ebrahim Raisi
Lakini kilichotokea jana ambacho hakikuwa cha kawaida ni kwamba ni wawakilishi kutoka Afrika, eneo la Asia-Pasifiki na Amerika ya Kusini tu pamoja na makundi ya kikanda ya eneo la Karibia waliozungumza.
Ulaya na Marekani zasusia kutoa heshima kwa Raisi
Hakukuwa na hotuba kutoka kwa mataifa ya Ulaya magharibi na mashariki, ama pia Marekani, ambayo kwa kawaida huzungumza ya mwisho ikiwakilisha nchi mwenyeji.