SiasaBrazil
Ulaya na Brazil kukamilisha makubaliano ya biashara
13 Juni 2023Matangazo
Von der Leyen aliyeko ziarani katika kanda ya Amerika Kusini,jana huko Brazil alikutana na rais Luiz Inacio Lula da Silva ambaye alikosoa kipengele kilichoongezwa na Umoja wa Ulaya katika mkataba huo,kutokana na wasiwasi wao juu ya kuharibiwa kwa msitu wa Amazon. Mkataba huo umekwama tangu mwaka 2019 kutoka wasiwasi huo wa Umoja wa Ulaya.
Nchi zinazohusika kwenye mkataba huo na Umoja wa Ulaya ni Brazil, Argentina, Paraguay na Uruguay.
Pamoja na kutangaza msaada wa euro bilioni 2 kwa Brazil kwa ajili ya kusimamia uzalishaji wa nishati ya Hydrogen isiyochafua mazingira, Von der Leyen amesifu uongozi wa rais Lula kuhusu sera yake ya mazingira na mpango wake wa kusitisha hatua ya kukatwa miti katika msitu wa Amazon kufikia mwaka 2030.