Ulaya kuipatia Ukraine risasi milioni 1
20 Machi 2023Matangazo
Nchi hizo pia zitapeleka haraka Ukraine risasi kutoka kwenye akiba zao zilizopo. Ukraine imeuambia Umoja wa Ulaya kwamba inahitaji makombora 350,000 kwa mwezi ili kuyasaidia majeshi yake kuzuia mashambulizi ya Urusi.
Soma pia: Umoja wa Ulaya waahidi kusimama na Ukraine bila kuchoka
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Catherine Colonna amesisitiza haja ya kuisaidia Ukraine zaidi, haraka na sasa. Makubaliano hayo yamefikiwa kutokana na wasiwasi kwamba Ukraine inaweza ikawa na uhaba wa aina muhimu zaa risasi katika siku zijazo.