1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Zelensky:Tutaendelea na usafirishaji nafaka bila Urusi

17 Julai 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema leo kwamba nchi yake iko tayari kuendelea na mauzo ya nafaka baada ya Urusi kujiondoa katika mkataba wa kihistoria uliosimamiwa na Uturuki na Umoja wa Mataifa.

https://p.dw.com/p/4U0i5
Ukraine I Volodymyr Selenskyj
Picha: Sergei Supinsky/AFP

Katika maoni yaliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na msemaji wake, Seriy Nykyforov, Zelensky amesema hata bila ya Shirikisho la Urusi, kila kitu kinapaswa kufanywa ili waweze kutumia njia ya Bahari Nyeusi.

Zelensky aliongeza kuwa hawaogopi na kwamba kampuni za usafirishaji zimewafuata na ziko tayari kuendelea na usafirishaji.

Soma pia:Urusi huenda isirefushe mpango wa usafirishaji nafaka

Katika hatua nyingine, Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen amesema leo kuwa uamuzi wa Urusi wa kuahirisha mkataba huo wa usafirishaji nafaka ni hatua isiyokuwa na maanana kuongeza kuwa Umoja huo utaendelea kufanya kazi katika kuhakikisha usalama wa chakula kwa nchi maskini.