Miji kadhaa ya Urusi yashambuliwa na Ukraine
17 Machi 2024Mashambulizi hayo ya Ukraine yamekilenga pia kiwanda cha kusafisha mafuta na kusababisha matatizo ya kukatika kwa umeme katika maeneo ya mpakani. Watu 7 wameripotiwa kuuawa katika mji wa Ukraine unaodhibitiwa na Urusi wa Kharkiv.
Gavana wa mkoa wa Belgorod Vyacheslav Gladkov amesema msichana wa miaka 16 ameuawa baada ya nyumba yake kushambuliwa na kombora kutoka Ukraine. Leo ikiwa ni siku ya mwisho ya upigaji kura nchini Urusi, Kremlin inaishutumu Kiev kujaribu kuhujumu mchakato wa uchaguzi.
Soma pia: Urusi inafanya uchaguzi katikati ya vita na Ukraine
Jeshi la Ukraine limetangaza kuwa mashambulizi ya anga ya Urusi yameharibu miundombinu ya viwanda vya kilimo katika bandari ya Odesa, huku Waziri wa ulinzi wa Urusi Sergei Shoigu akilimuru hii leo jeshi la wanamaji kuimarisha ulinzi katika Bahari Nyeusi.