1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUrusi

Ukraine yailenga Urusi kwa zaidi ya droni 140

10 Septemba 2024

Maafisa wa Urusi wameripoti mapema leo kuwa, zaidi ya droni 140 za Ukraine zimeilenga mikoa chungu nzima ya Urusi usiku wa kuamkia leo, ukiwemo mji mkuu wa Moscow na maeneo ya jirani.

https://p.dw.com/p/4kS5S
Ramenskoye Urusi | Mashambulizi ya droni
Moja ya jengo lililoharibiwa vibaya na mashambulizi ya dfoni yanayodaiwa kufanywa na Ukraine karibu na Moscow Picha: Sergei Bulkin/TASS/dpa/picture alliance'

Hilo ni moja ya shambulio kubwa zaidi la ndege za droni kufanywa na Ukraine kwenye ardhi ya Urusi katika vita vya zaidi ya miaka miwili.

Gavana wa mkoa wa Moscow Andrei Vorobyov amesema kuwa majengo mawili ya makazi katika mji wa Ramenskoye nje kidogo ya Moscow, yalishambuliwa na ndege za droni na kisha kuwaka moto.

Shambulio hilo pia limesababisha mamlaka kuvifunga kwa muda viwanja vya ndege vitatu nje ya Moscow. Kulingana na taarifa ya wizara ya ulinzi ya Urusi, kiasi cha ndege 144 za droni za Ukraine zimedunguliwa katika jumla ya mikoa tisa ya Urusi