1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ukraine yadungua droni 15 za Urusi

29 Agosti 2024

Kikosi cha anga cha Ukraine kimedungua trakiban droni 15 za Urusi kwenye mji mkuu, Kiev.

https://p.dw.com/p/4k32f
Ukraine-Krieg - Krieg der Drohnen | Russische Drohne
Picha: Andrei Rubtsov/Tass/dpa/picture alliance

Mkuu wa utawala wa kijeshi wa Kiev, Serhiy Popko amesema leo kuwa hilo ni shambulizi la tatu mjini Kiev, katika muda wa siku nne.

Gavana wa Kiev, Ruslan Krwavchenko amesema droni hizo hazijasababisha uharibifu wowote kwenye miundombinu muhimu ya Kiev.

Krwavchenko amesema maafisa wa mji na jimbo hawajaripoti madhara yoyote yale.

Wakati huo huo, Gavana wa Belgorod Vyacheslav Gladkov, amesema raia mmoja ameuawa na wengine wawili wamejeruhiwa katika shambulizi la kombora la Ukraine kwenye mji wa Shebekino, katika jimbo hilo la Urusi.

Aidha, Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky amesema shambulizi la anga la Urusi limewaua watu kadhaa katika mji wa Kupyansk.

Zelensky amewataka viongozi wa mataifa ya Magharibi kuiruhusu Ukraine kutumia silaha za Magharibi kwa ajili ya mashambulizi ya masafa marefu.