1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine: Urusi inaishikilia Belarus kama mateka wa nyuklia

26 Machi 2023

Serikali ya Ukraine imesema leo kuwa Moscow inaishikilia Minsk kama "mateka wa nyuklia" baada ya Rais wa Urusi Vladimir Putin kutangaza kutuma silaha za kimkakati za nyuklia kwa washirika wake Belarus.

https://p.dw.com/p/4PG4F
Ukraine Kiew | Sekretär des Nationalen Sicherheits- und Verteidigungsrats der Ukraine Oleksij Danilow
Picha: Anna Voitenko/REUTERS

Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa Baraza la Usalama na Ulinzi la Kitaifa la Ukraine, Oleksiy Danilov, kupitia ukurasa wake katika mtandao wa kijamii wa Twitter, akiongeza kuwa hiyo ni "hatua ya kudhoofisha utulivu wa ndani wa nchi hiyo".

Shirika la habari la Tass lilimnukuu Rais Vladimir Putin akisema kuwa Urusi ilifikia makubaliano na jirani yake Belarus ili kupeleka silaha za kimkakati za nyuklia.

Soma pia: Viongozi wa Ulaya kuharakisha kuipatia Ukraine silaha

Hata hivyo, Idara ya Ulinzi ya Marekani imesema hakuna dalili zozote kwamba Urusi inajiandaa kutumia silaha za nyuklia baada ya tangazo hilo.