1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Ukraine kupokea magari zaidi ya kivita

5 Januari 2023

Washirika wa magharibi wa Ukraine wamefikia uamuzi wa kusambaza magari ya kivita kwa Ukraine huku Marekani ikitabiri kwamba mapigano makali yataendelea kwa miezi kadhaa upande wa mashariki.

https://p.dw.com/p/4LlSB
Norwegen | NATO Manöver Cold Response 22
Picha: Geir Olsen/NTB/AFP/Getty Images

Kwa mujibu wa afisa wa serikali ya Ufaransa, Rais Emmanuel Macron amemwambia mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy kwamba serikali yake itapeleka magari ya kivita aina ya AMX-10 RC nchini Ukraine kusaidia katika vita dhidi ya Urusi.

Afisa huyo amesema magari hayo ya kivita ndio ya kwanza kutumwa kutoka Magharibi lakini Australia ilisema Oktoba kwamba imeipa Kyiv magari 90 ya kujihami ya kivita ambayo yameimarishwa dhidi ya mabomu ya ardhini, milipuko ya silaha ndogo ndogo na vitisho vingine.

Zelenskiy alimshukuru Macron kwa tangazo hilo na kusema lilionyesha hitaji la washirika wengine kutoa silaha nzito zaidi.

Rais wa Marekani Joe Biden amesema kwamba Washington inafikiria kutuma magari ya Kivita ya Bradley nchini Ukraine.