Asili na mazingiraZimbabwe
Ukosefu wa maji walazimisha Tembo kuihama Zimbabwe
19 Septemba 2023Matangazo
Hayo yameelezwa na msemaji wa Mamlaka ya Hifadhi za Taifa za Zimbabwe, Tinashe Farawo, ambaye amearifu kuwa Ndovu hao walianza kuhama tangu mwezi Agosti na wanaelekea nchini Botswana baada ya vyanzo vya maji kwenye mbuga ya wanyama ya Hwange nchini Zimbabwe.
Inaaminika sababu za kukauka kwa vyanzo vya maji ni athari za mabadiliko ya tabianchi.
Farawo amesema idadi ya tembo wanaohama ni kubwa na kuna mashaka watalazimika kupita kwenye maeneo yenye shughuli nyingi za binadamu.
Mwaka uliopita pekee tembo walisababisha vifo vya watu 60 nchini Zimbabwe, takwimu zinazoakisi ongezeko la muingiliano baina ya watu na wanyama hao wa mwituni.