Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wawasili DRC
10 Machi 2023Matangazo
Ujumbe huo leo unatarajiwa kukutana na Rais Felix Tshisekedi kabla ya kuelekea Goma kesho Jumamosi. Kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Kongo, MONUSCO, kimesema lengo la ziara hiyo ni kutathmini hali ya usalama na kiutu Kivu Kaskazini.
Baada ya kuwasili Kinshasa, Balozi wa Gabon katika Umoja wa Mataifa Michel Xavier Biang, alisema wako Kongo kwa ajili ya kuunga mkono shughuli za MONUSCO, na kukumbusha kuwa ni sehemu ya kutafuta amani.
Wakaazi wa mashariki mwa Kongo waneishutumu MONUCSO kwa kushindwa kukabiliana na makundi kadhaa yenye silaha kwenye eneo hilo.