1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujumbe wa Sudan kwenye mazungumzo ya Jeddah warejea

27 Julai 2023

Taarifa ya jeshi la Sudan imesema ujumbe wa jeshi hilo katika mazungumzo ya amani yanayofanyika Jeddah, Saudi Arabia, umerudi nyumbani kwa ajili ya mashauriano.

https://p.dw.com/p/4UUBb
Suadan | General Abdel Fattah al-Burhan in Khartum
Picha: Sudanese Armed Forces/AA/picture alliance

Taarifa hiyo imesema ujumbe huo utarudi kwenye mazungumzo hayo mara baada ya vigingi vilivyoko kusawazishwa.

Jeshi hilo limesema tofauti katika masuala kadhaa ikiwemo waasi kuwaokoa raia majumbani na katika mashirika ya umma, hospitali na bararani, ndiyo mambo yaliyopelekea hatua ya kutoelewana.

Soma zaidi: Raia wa Sudan wazidi kuyakimbia mapigano

Haya yanafanyika wakati ambapo kumeripotiwa mashambulizi ya maroketi katika mji mkuu Khartoum leo, wakati wapiganaji wa RSF walipoishambulia kambi muhimu ya jeshi la angani na kudai kuwauwa wanajeshi kadhaa.

RSF imeripoti kuwa imeharibu ndege tatu za kivita, pamoja na hifadhi ya silaha.