SiasaKorea Kaskazini
Mawaziri wa Korea Kaskazini kuanza ziara nchini Iran
24 Aprili 2024Matangazo
Mataifa hayo yamekuwa yakishukiwa kuwa na mahusiano ya siri ya kijeshi. Taarifa hiyo imetolea na shirika la habari la serikali ya Korea Kaskazini KCNA.
Waziri anayehusika na mahusiano ya kiuchumi wa Korea Kaskazini Yun Jong Ho, ameondoka jana mjini Pyongyang kuelekea Iran akiongozana na mawaziri wengine kadhaa. Hata hivyo vyombo vya habari nchini humo havikutoa taarifa zaidi.
Korea Kaskazini na Iran kwa muda mrefu zimekuwa zikishukiwa kushirikiana kwenye programu za makombora ya masafa marefu, na pia kubadilishana utaalamu wa kiufundi na hata vifaa vinavyotumiwa katika utengenezaji wa silaha hizo.
Mataifa hayo mawili yamekuwa yakishutumiwa pia kuisaidia Urusi katika uvamizi wake nchini Ukraine kwa kuipatia makombora na silaha zingine.