1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujumbe wa Israel waondoka Cairo bila ya kupatikana mafanikio

14 Februari 2024

Vyombo vya habari vya Israel na Marekani vimeripoti kwamba ujumbe wa Israel umeondoka katika mazungumzo ya mjini Cairo ya kusitisha vita kati ya Israel na kundi la Hamas.

https://p.dw.com/p/4cO6V
Rafah, Ukanda wa Gaza | Mwanamke akilia katikati ya mashambulizi ya Israel
Mkaazi wa gaza akilia huku Israel ikivurumisha mkururo wa mashambuliziPicha: IBRAHEEM ABU MUSTAFA/REUTERS

Mazungumzo juu ya kusimamisha mapigano kwenye Ukanda wa Gaza yamemalizika bila ya kufikiwa mapatano. Mazungumzo hayo yalifanyika mjini Cairo na yalihudhuriwa na wajumbe kutoka Misri, Israel, Qatar na Marekani iliyowakilishwa na mkurugenzi wa shirika la ujasusi, CIA bwana William Burns na Israel iliwakilishwa na mkuu wa shirika la ujasusi la Israel David Barnea.

Soma pia:Mazungumzo ya kusitisha mapigano Gaza 'yafika pazuri'

Wakati huo huo miito juu ya kuitaka Israel ighairi mpango wa kuushambulia mji wa Rafah inaendelea kutolewa kwa sauti kubwa zaidi.

Watu zaidi ya milioni mojawanasongamana kwenye mji huo wa kusini mwa Ukanda wa Gaza ambapo nusu ya watu hao ni wale waliokimbia makazi yao kutoka sehemu zingine za Ukanda wa Gaza.