1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujumbe wa ECOWAS wawasili Niger

2 Agosti 2023

Wajumbe kutoka jumuiya ya kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS wamewasili Niger ili kujadiliana na utawala wa kijeshi, wiki moja tu baada ya mapinduzi kuzua hali ya wasiwasi miongoni mwa nchi jirani na washirika.

https://p.dw.com/p/4UhEa
ECOWAS Meeting
Picha: Xinhua News Agency/picture alliance

Vyanzo kutoka jumuiya hiyo na afisa wa jeshi la Nigeria wameliambia shirika la habari la AFP kuwa wajumbe hao wanaoongozwa na rais wa zamani wa Nigeria Abdulsalami Abubakar watasafiri kuelekea mji mkuu Niamey leo Jumatano.Wakuu wa jeshi la jumuiya hiyo pia wanatarajiwa kuanza mkutano wa siku tatu utakaofanyika katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja kujadili juu ya hali ya mambo nchini Niger.Mnamo siku ya Jumapili, viongozi wa ECOWAS waliamua kuiwekea Niger vikwazo vya kibiashara na kifedha na kuwapa viongozi wa mapinduzi muda wa wiki moja kumrejesha madarakani rais Mohamed Bazoum la sivyo wakabiliwe kijeshi.Hata hivyo, Mali na Burkina Faso zilizoko chini ya utawala wa kijeshi zimeonya kuwa uingiliaji wa kijeshi nchini Niger ni sawa na kutangaza vita dhidi yao.