Ujerumani yahimiza kufanyika juhudi kuzuia migogoro
29 Julai 2024Matangazo
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani amesema shambulio hilo linaloaminika kufanywa na kundi la Hezbollah pamoja na vitendo vya hivi karibuni vya wanamgambo wa Kihouthi wa Yemen yamechangia hali mbaya ya uthabiti katika eneo hilo.
Makundi ya Hezbollah na Wahouthi yote wanaungwa mkono na Iran.
Soma pia: Baerbock afanya ziara Ivory Coast baada ya Senegal
Kwa mujibu wa msemaji huyo wa wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani waziri Annalena Baerbock amefanya mazungumzo na viongozi kadhaa wa Lebanon ikiwemo waziri mwenzake wa mambo ya nje kujaribu kuzuia kutanuka kwa mgogoro huo.
Ujerumani pia imewashauri raia wake takriban 1,300 walioko Lebanon waondoke wakati huu ambapo bado hali inaruhusu.