1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yatangaza mabadiliko ya sheria ya mazingira

15 Juni 2023

Baada ya miezi kadhaa ya majadiliano, serikali ya Ujerumani imetangaza kurekebisha sheria yake ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambayo imekuwa ikitumika kama msingi wa sera yake kwa serikali ya shirikisho.

https://p.dw.com/p/4SacH
Ujerumani| Berlin | Robert Habeck
Waziri wa Uchumi na dhamana ya mabadiliko ya tabia wa Ujerumani Robert HabeckPicha: Florian Gaertner/photothek/IMAGO

Baada ya miezi kadhaa ya majadiliano, serikali ya Ujerumani imetangaza kurekebisha sheria yake ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambayo imekuwa ikitumika kama msingi wa sera yake kwa serikali ya shirikisho.

Waziri wa Uchumi na dhamana ya mabadiliko ya tabia nchi kutoka chama cha walinzi wa mazingira Robert Habeck, ambae amesimamia sheria hiyo amesema lengo ni kupunguza uzalishaji wa hewa chafu kwa asilimia 65 ifikapo 2030.

Soma: Polisi Ujerumani wawahamisha wanaharakati kupisha mgodi wa makaa

Pamoja na mabadiliko hayo kuanza mwaka 1990 Ujerumani ilikuwa inapaswa kupunguza hewa ya ukaa kutoka kiwango hicho cha asalimia 65 ifikapo 2030.

Hata hivyo serikali bado ipo katika tafakari ya juu ya namna gani, katika sekta zipi na kiasi gani kitaruhusiwa ili kufanikisha lengo la mwaka 2030.