Ulimwengu uachane na matumizi ya makaa ya mawe na mafuta
5 Desemba 2023Matangazo
Wajumbe kwenye mkutano huo wameeleza kwamba Ujerumani imekabiliwa na upinzani wa serikali nyingi kati ya 200 zinazoshiriki mkutano huo wa kilele mjini Dubai. Mjumbe maalum wa Ujerumani katika mkutano huo Jennifer Morgan amesema lengo kuu la nchi yake liko wazi na ambalo ni kuunga mkono nishati mbadala.Waziri wa nishati wa Saudi Arabia, AbdulAziz bin Salman ni miongoni mwa wanaopinga kabisa mpango huo wa pamoja wa makubaliano ya kuondokana na nishati ya makaa ya mawe,mafuta na gesi. Amezishutumu nchi zinazoshinikiza mpango huo wa kuondokana na matumizi ya nishati ya visukuku kuwa na undumilakuwili.