Ujerumani yaondoa sharti la ukomo wa kukopa kwa mwaka 2023
15 Desemba 2023Matangazo
Hii ni sehemu ya jibu la bunge la Ujerumani kwa uamuzi uliotolewa na mahakama ya katiba katikati ya mwezi Novemba kuwa, fedha zilizotengwa wakati wa janga la UVIKO-19 hazipaswi kutumiwa kwa ajili ya miradi ya mazingira na ruzuku kwa nishati.
Kuondolewa kwa marufuku hiyo ya "ukomo wa deni" inafungua njia kwa serikali ya Ujerumani kuidhinisha bajeti ya ziada, ambayo itapigiwa kura baadaye leo.
Deni jipya sasa litafikia jumla ya euro bilioni 70.61 ambacho ni kiasi cha euro bilioni 44.8 juu ya kikomo kinachoruhusiwa kukopwa.
Bunge la Ujerumani sasa linasitisha kwa mara ya nne mfululizo utekelezwaji wa sheria ya ukomo wa deni.