Ujerumani yamwita balozi wa Iran kufuatia shambulizi Israel
15 Aprili 2024Iran imesema hatua iliyochukuliwa inaonesha misimamo isiyowajibika ya Ujerumani, Ufaransa na Uingereza ambazo zote zimewaita mabalozi wa Iran katika nchi zao kujadili shambulio hilo.
Italia nayo inayoshikilia urais wa kupokezana wa kundi la nchi tajiri kiviwanda la G7 imesema kupitia waziri wake wa mambo ya nje Antonio Tajani, kwamba iko tayari kwa hatua ya kuwawekea vikwazo watu binafsi watakaohusika na mashambulizi dhidi ya Israel.
Kwa mara ya kwanza katika historia, Iran imeishambulia moja kwa moja adui yake wa miaka mingi Israel kwa droni zaidi ya 300 pamoja na kuifyetulia makombora yaliyofanikiwa kudunguliwa kwa asilimia 99.
Iran ilikuwa inajibu shambulizi linalodaiwa kufanywa na Israel katika ubalozi wake mdogo nchini Syria lililosababisha mauaji ya makamanda wake.