MigogoroMashariki ya Kati
Ujerumani yalaani ongezeko la ghasia dhidi ya UNRWA
10 Mei 2024Matangazo
Ujerumani imelaani ongezeko la ghasia dhidi yaShirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi wa Kipalestina UNRWA, huko Jerusalem Mashariki, baada ya shirika hilo kuzifunga ofisi zake kwa muda kufuatia mashambulizi ya mara kwa mara.
Wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani imeandika kupitia ukurasa wa mtandao wa X kwamba Israel inapaswa kuhakikisha ulinzi wa vituo vya Umoja wa Mataifa na wafanyakazi wake katika eneo linalokaliwa la Wapalestina.
Mkuu wa Shirika la UNRWA, Philippe Lazzarini alitangaza siku ya Alhamisi kwamba wanafunga kwa muda ofisi zao, baada ya Waisraeli kuchoma moto karibu na maeneo ya ofisi za shirika hilo, katika mashambulizi ya hivi karibuni. Mamlaka ya Palestina, Jordan na Saudi Arabia nazo pia zililaani ghasia hizo.