Ujerumani yajiunga na Kamandi ya Umoja wa Mataifa, UNC
2 Agosti 2024Matangazo
Pistoriusamesema kuwa sasa Ujerumani inalenga kuchangia katika uthabiti wa kanda hiyo. Waziri huyo wa ulinzi ameongeza kuwa Berlin itajadiliana na washirika wa kamandi hiyo katika kambi ya kijeshi ya Pyeongtaek, jinsi inavyoweza kutoa mchango wake kama mwanachama wa 18. Kamandi hiyo ya Umoja wa Mataifa ina jukumu la kuhakikisha kwamba maelewano ya usitishwaji wa mapigano wakati wa vita vya Korea vilivyofanyika kati ya mwaka 1950 na 1953 yanafuatwa.