1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yaitahadharisha China dhidi ya kuisaidia Urusi

2 Desemba 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock amemtahadharisha mwenzake wa China Wang Yi dhidi ya kuisaidia Urusi katika mzozo wake na Ukraine.

https://p.dw.com/p/4neqI
Beijing China | Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena BAerbock (Kushoto) akiwa na mwenzake wa China Wang YI mjini BeijingPicha: Michael Kappeler/dpa/picture alliance

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock amemtahadharisha mwenzake wa China Wang Yi kwamba uungaji mkono wa Beijing kwa Moscow utaathiri mahusiano baina ya nchi hizo mbili, huku akiitaka China kusaidia kuumaliza mzozo wa Ukraine.

Akizungumza akiwa ziarani mjini Beijing, Baerbock amesema vita vya zaidi ya siku 1,000 nchini Ukraine vinaithiri dunia nzima, huku akilaani jukumu la wanajeshi wa Korea Kaskazini na matumizi ya droni zilizotengenezwa na China katika mzozo huo.

Baerbock amehimiza kuwepo kwa mchakato wa kimataifa wa amani kwa ajili ya Ukraine na kuongeza kuwa kila mwanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ana wajibu wa kudumisha amani na usalama duniani. China ambayo ni mshirika wa Urusi, imekuwa ikidai kutoegemea upande wowote katika mzozo huo.