1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani na msimamo wa vifaru vya Leopard kupelekwa Ukraine

23 Januari 2023

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Annalena Baerbock amesema Ujerumani haitaiwekea pingamizi Poland ikiwa inataka kutuma vifaru vya kivita chapa ya Leopard nchini Ukraine.

https://p.dw.com/p/4MZcd
Deutschland Bundeswehr Kampfpanzer Leopard 2 A7V
Picha: Philipp Schulze/dpa/picture-alliance

Hiyo ni ishara inayoonesha uwezekano wa mafanikio kwa Ukraine, wakati ikijaribu kuimarisha vikosi vyake kuelekea mashambulizi mapya yanayotarajiwa ya Urusi. 

Kwa miezi kadhaa maafisa wa Ukraine wamekuwa wakizitolea wito nchi washirika wa Magharibi kuipatia nchi hiyo vifaru vya kisasa kutoka Ujerumani.

Lakini Ujerumani imejiuzuwia kutuma vifaru hivyo au kuruhusu mataifa mengine wanachama wa Jumuia ya Kujihami ya NATO kufanya hivyo.

Vifaru aina ya Leopard ambavyo mataifa kadhaa ya NATO yanavyo, lakini ambavyo uhamishwaji wake nchini Ukraine unahitaji idhini ya Ujerumani, vinatazamwa na wataalamu wa ulinzi kama vinavyofaa zaidi kwa Ukraine.