Ujerumani, Ufaransa na Poland kujadili masuala ya usalama
22 Mei 2024Matangazo
Hayo ni kwa mujibu wa msemaji wa ofisi ya mambo ya nje ya Ujerumani iliyopo Berlin aliyeongeza kuwa masuala mengine yatakayopewa kipaumbele katika mazungumzo hayo ni Vita vya Urusi na Ukraine, na muelekeo wa siku za usoni wa Umoja wa Ulaya pamoja na mzozo wa Mashariki ya kati.
Baerbock atakutana na wenzake baada ya kurejea nchini hii leo kutoka Ukrainealikotoa wito wa usaidi zaidi wa kimataifa kwa Ukraine. Viongozi wa Ujerumani, Ufaransa na Poland hukutana mara kwa mara chini ya mwamvuli wa muungano wa Weimar ulioundwa mwaka 1991.