1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani: Posho za wasio na kazi kuongezwa.

29 Agosti 2023

Posho za watu wasiokuwa na ajira zitaongezwa hadi euro 609 kwa mwezi kuanzia mwaka ujao nchini Ujerumani kulinganisha na malipo ya sasa ya Euro 502.

https://p.dw.com/p/4ViDR
Waziri wa ajira nchini Ujerumani Hubertus Heil
Waziri wa ajira nchini Ujerumani Hubertus HeilPicha: Fabian Sommer/dpa/picture alliance

Waziri wa ajira Hubertus Heil amesema watu zaidi ya milioni tano watanufaika na ongezeko hilo la asilimia 12.

Waziri huyo ameeleza kuwa watu hapa nchini Ujerumani wanaweza kuitegemea serikali inayojali ustawi wa jamii na hasa katika nyakati za shida na misukosuko.

Serikali ya mseto ya Ujerumani ilipitisha mageuzi makubwa katika mfumo wa ustawi wa jamii mwaka uliopita kwa manufaa  ya watu ambao wamekaa muda mrefu bila ya ajira.

Mageuzi hayo pia yanalenga kutoa mafunzo bora zaidi ya kujipatia ujuzi kwa watu wasiokuwa na ajira.

Posho kwa ajili ya watu wenye watoto pia zinatarajiwa kuongezwa.