Ujerumani na EU zalaani kunyongwa kwa Jamshid Sharmahd
29 Oktoba 2024Matangazo
Ujerumani na Umoja wa Ulaya zimesema zinatafakari hatua za kulipiza kisasi.
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema kunyongwa Sharmahd ni "kashfa" na Waziri wa Mambo ya Nje Annalena Baerbock ameuonya utawala wa Iran kwamba utajibiwa vikali.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amejibu kupitia mtandao wa kijamii wa X akisema "Pasipoti ya Ujerumani haimfanyi mtu yeyote aepuke adhabu, na hasa mhalifu na gaidi".
Iran yamnyonga Jamshid Sharmahd raia wa Ujerumani na Iran
Ujerumani imewasilisha malalamiko yake kwa Iran. Balozi wa Ujerumani mjini Tehran pia aliwasilisha malalamiko kwa wizara ya mambo ya nje ya Iran na kisha alirudishwa Berlin kwa mashauriano.