1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
UchumiUjerumani

Ujerumani na Ukraine zafanya mkutano wa kiuchumi Berlin

11 Desemba 2024

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema Rais Vladmir Putin wa Urusi ameshindwa kufanikiwa kutimiza lengo hata moja kati ya malengo yake yaliyompeleka vitani Ukraine.

https://p.dw.com/p/4o0sW
Mkutano wa kiuchumi kati ya Ujerumani na Ukraine mjini Berlin | Olaf Scholz
Mkutano wa jukwaa la kiuchumi baina ya Ujerumani na Ukraine, unalenga kutazama uwezo wa kiuchumi wa Ukraine baada ya miaka mitatu ya uvamizi wa UrusiPicha: John MacDougall/AFP/Getty Images

Kiongozi huyo wa Ujerumani pia amesema mpango wa kuikaribisha Ukraine katika  Umoja wa Ulaya hauwezi kuondolewa.

Scholz ameyasema hayo mjini Berlin ambako unafanyika

Mkutano wa jukwaa la kiuchumi baina ya Ujerumani na Ukraine, ukilenga kutazama uwezo wa kiuchumi wa Ukraine baada ya takriban miaka mitatu ya vita kamili vilivyosababishwa na uvamizi wa Urusi.

Katika mkutano huo suala la usambazaji nishati na ushirikiano wa makampuni ya silaha ya Ujerumani na Ukraine yatapewa kipaumbele.

Kansela Olaf Scholz,waziri wa uchumi Robert Habeck na waziri wa maendeleo Svenja Schulze wanashiriki mkutano huo.

Ukraine inawakilishwa na waziri mkuu Denys Shmyhal na naibu wake Yulia Svydenko na waziri wa nishati Herman Halushchenko.