1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani na New Zealand zasaini mkataba wa ushirikiano

Saleh Mwanamilongo
4 Mei 2024

Hatua hiyo imefikiwa leo Jumamosi wakati wa ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Annalena Baerbock mjini Auckland.

https://p.dw.com/p/4fVG3
Ujerumani na New Zealand zimetia saini mkataba wa maelewano ya kukuza ushirikiano baina yao
Ujerumani na New Zealand zimetia saini mkataba wa maelewano ya kukuza ushirikiano baina yaoPicha: Florian Gaertner/photothek/IMAGO

Waziri wa Mambo ya Nje wa New Zealand, Winston Peters, amesema mkataba huo utaongeza uhusiano kati ya Ujerumani na New Zealand.

Mawaziri hao wawili pia walijadili haja ya kusitishwa kwa mapigano mara moja huko Gaza na kuimarisha ushirikiano katika eneo la Pasifiki. Peters alisema New Zealand na Ujerumani zinaamini kwenye maslahi na maadili ya pamoja, ikiwa ni pamoja na utawala wa sheria, demokrasia, heshima kwa mfumo wa kimataifa na haki za binaadamu.

Annalena Baerbock aliwasili New Zealand jana Ijumaa kutoka Australia. Hapo kesho Jumapili, Baerbock atatembelea kisiwa cha Fiji katika Pasifiki ya Kusini.