Ujerumani kuweka masharti magumu ili kuzuia uhamiaji
7 Novemba 2023Matangazo
Muafaka huo umepatikana mjini Berlin katika jambo ambalo limekuwa tatizo kubwa la kisiasa na kijamii.
Hatua hizo mpya zitajumuisha msaada wa kifedha kwa majimbo ili kukabiliana na suala la uhamiaji pamoja na kuharakisha mchakato wa kuomba hifadhi nchini Ujerumani.
Scholz ambaye amekuwa akikabiliwa na shinikizo kutoka kwa upinzani, ameyaelezea makubaliano hayo kuwa ya kihistoria.
Hadi mwishoni mwa mwezi Septemba, idadi ya waomba hifadhi imeongezeka nchini Ujerumani kwa asilimia 73 ukilinganisha na kipindi hicho mwaka uliopita.
Ujerumani imewapokea pia Waukraine zaidi ya milioni 1 tangu Urusi ilipoanzisha uvamizi wake nchini humo.