1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani kulegeza msimamo kuhusu mageuzi ya uombaji hifadhi

28 Septemba 2023

Serikali ya Ujerumani imesema ipo tayari kukubali pendekezo jipya kuhusu udhibiti wa uhamiaji kuingia Umoja wa Ulaya wakati wa migogoro.

https://p.dw.com/p/4WvQh
Nancy Faeser, waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani
Nancy Faeser, waziri wa mambo ya ndani wa UjerumaniPicha: Maja Hitij/Getty Images

Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Nancy Faeser aliyezungumza leo mjini Brussels kwenye mkutano wa mawaziri wa mambo ya ndani wa umoja huo amesema, nchi yake sasa iko tayari kupigia kura pendekezo linalojadiliwa la mageuzi ya mfumo wa Umoja wa Ulaya kupunguza waomba hifadhi.

Ujerumani ilikataa pendekezo la mwezi Julai na imekuwa ikitoa wito wa mara kwa mara wa ulinzi bora kwa familia chini ya pendekezo hilo.

Idadi ya wahamiaji wanaofika katika Umoja wa Ulaya imeongezeka pakubwa katika miezi ya hivi karibuni, na kufichua mivutano ambayo haijatatuliwa kuhusu suala hilo kati ya nchi 27 wanachama wa umoja huo.