1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani kuharakisha uondoaji wa wanajeshi wake Mali

Sylvia Mwehozi
28 Juni 2023

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius amekiambia kituo cha utangazaji cha umma ZDF leo, kuwa Ujerumani inatazamia kuondoa wanajeshi wake kutoka Mali haraka iwezekanavyo.

https://p.dw.com/p/4T9Zc
Bundeswehr Soldaten des Jägerbataillon 292
Wanajeshi wa Ujerumani wakifanya mazoezi katika kituo cha Letzlingen.Picha: Florian Gaertner/photothek/IMAGO

Pistorius amesisitiza kwamba zoezi la kuondoa wanajeshi hao litafanyika kwa namna inayozingatia utaratibu.

Waziri huyo wa ulinzi wa Ujerumani amesema uondoaji utaharakishwa kwa muktadha wa mwisho unaopangwa wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa hapo Juni 30.

Ujerumani ambayo ina wanajeshi wapatao 1,000 nchini Mali, tayari ilianza mchakato wa kuondoa vikosi vyake na inalenga kukamilisha mchakato huo kufikia Mei 2024.