1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani inahitaji kuongeza wanajeshi

12 Oktoba 2024

Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ya bunge la Ujerumani, Marcus Faber amesema jeshi la nchi hiyo linahitaji wanajeshi wengine zaidi wasiopungua 35,000 ili kukidhi mahitaji mapya ya ulinzi ya Jumuiya ya Kujihami ya NATO.

https://p.dw.com/p/4liGD
Wanajeshi wa Ujerumani katika wakiwa mafunzoni
Wanajeshi wa UjerumaniPicha: Thomas Koehler/photothek/picture alliance

Faber ameunga mipango ya kuongeza idadi ya vikosi vya wanajeshi wa Ujerumani katika Jumuiya ya kujihami ya NATO kutoka 82 hadi 131 kuanzia mwaka 2031. Ametoa kauli hiyo ikiwa ni hatua ya kuunga mkono miito ya kuwa na jeshi kubwa zaidi ili kukabiliana na vitisho vya kiusalama vinavoongezeka kutoka Urusi.

Soma zaidi: Jeshi la Ujerumani lina utayari kubeba dhamana NATO?

Akizungumza na shirika la habari la Redaktionsnetzwerk Deutschland (RND) Faber ameeleza kuwa badala ya kuwa na divisheni tatu za kijeshi zenye wanajeshi 65,000, Ujerumani itahitaji divisheni nne zitakazokuwa na takriban wanajeshi 100,000.

Mpango huo unatarajiwa kuchukua muda wa miaka 10 hadi kukamilika.  Kwa sasa jeshi la Ujerumani, Bundeswehr, lina jumla ya wanajeshi 180,000 pekee.