1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani imejiandaa vipi kwa EURO 2024

14 Juni 2023

Michuano ya kuwania kombe la Ulaya la 2024 inatazamiwa kuanza nchini Ujerumani mwaka mmoja kutoka sasa. Hali ni tofauti kabisa na Kombe la Dunia la 2006, mara ya mwisho Ujerumani ilipoandaa mashindano makubwa.

https://p.dw.com/p/4SZQE
Fußball Deutschland Nationalmannschaft | Hansi Flick und Danny Röhl
Picha: Laci Perenyi/IMAGO

Masuala yanayoendelea katika kikosi cha Ujerumani yaliibuka tena katika sare ya 3-3 ya dhidi ya Ukraine siku ya Jumatatu, mechi ya 1,000 katika historia ya timu ya taifa ya kandanda ya wanaume. Kulikuwa na makosa kadhaa, kupoteza nafasi za wazi, huku wachezaji wakijitahidi kupata ujasiri wao.

Changamoto kubwa zaidi ipo kwenye ulinzi, udhaifu unaoendelea. Mabeki wa Ujerumani hawawezi kustahimili mashambulizi na mipira mirefu ya juu kama walivyokuwa wakati wa Kombe la Dunia la 2022 nchini Qatar na pia walipopoteza 3-2 dhidi ya Ubelgiji katika mechi yao ya mwisho ya kirafiki ya kimataifa. Changamoto hii imetokana na wachezaji kufanya makosa binafsi ya kushangaza.

Katika ushambuliaji mambo hayakuwa rahisi, safu ya ulinzi ya Ukraine ilijipanga vyema, ushambuliaji wa kikosi cha Hansi Flick ulikuwa mbaya na ulitoa nafasi kwa wapinzani kutumia fursa.

Tatizo kubwa zaidi ni kwamba kikosi cha Ujerumani hakina wabeki wengi na pia hawana mshambuliajia wa kiwango cha kimataifa wa kujivunia kama ilivyo kwa mataifa mengine. Licha ya kwamba safu ya kati ina wachezaji wa hali ya juu bado kuna mapungufu.

Walipocheza na Ukraine, Kocha Flick aliwategemea viungo Leon Goretzka, Joshua Kimmich na Julian Bradt lakini walishinda kupenya na kutoa matokeo. Flick anajukumu la kutafuta mfumo na wachezaji sahihi wakati akiendelea kubeba jukumu la kubanduliwa katika hatua ya makundi wakati wa Kombe la Dunia. Timu ya Ujerumani inahitaji muundo, kujiamini na nia dhabiti ya ushindi.

Inadhihirika wazi miongoni mwa umma hasa wakati matokeo ya kikosi cha timu ya taifa yanaondoa motisha ya ushabiki. Ujerumani, iko chini ya kiwango cha kuridhisha na hakuna dalili ya furaha yoyote ya Ubingwa wa Ulaya nyumbani.

"Kandanda inategemea matokeo na matokeo ndio msingi, na tunapaswa kushikilia matokeo haraka iwezekanavyo," alisema Kimmich, nahodha wa Ujerumani. "Tunahitaji ushindi."

Ni nini kimefanikiwa vizuri kwa Ujerumani?

Fussball WM 2022 I DFB Training Katar
Picha: Markus Gilliar/GES/picture alliance

Flick alitangaza baada ya Kombe la Dunia kuwa anataka kubadilisha baadhi ya wachezaji. Tayari amewapa baadhi ya nyuso mpya nafasi ya kujidhihirisha, lakini bila muundo wowote, hakuna anayeweza kuwa na uhakika wa nafasi yake kwenye timu. Chanya ni kwamba Flick bado ana mwaka mzima wa kubadilisha mfumo wake na kutafuta wachezaji wanaoufaa.

Mshambulizi Niclas Füllkrug, ambaye mara kwa mara amekuwa akifanya vyema na kufunga mabao. Bao lake la kwanza dhidi ya Ukraine lilimweka katika kundi la wachezaji wa kimataifa wa Ujerumani ambao wamefunga katika mechi tano mfululizo. Iwapo atafunga katika mchezo unaofuata wa Ujerumani nchini Poland, atakuwa mchezaji wa kwanza wa timu ya taifa ya Ujerumani kusajili mabao sita katika mechi mfululizo.

Vijana wenye vipaji kama Florian Wirtz, ambaye hivi majuzi alipona jeraha la goti, na Jamal Musiala wanadhihirisha uwezekano wa kuimarika.

Je, njia ya Ujerumani kuelekea EURO 2024 ni ipi?

Fußball Deutschland Nationalmannschaft | Assistenztrainer Danny Röhl
Picha: Marc Schüler/IMAGO

Mechi mbili za kirafiki za kimataifa zimesalia mwezi Juni, na tatu zimepangwa mnamo Septemba na Oktoba. Kikosi cha Ujerumani kina mapumziko mafupi tu kabla ya mtihani mgumu zaidi dhidi ya Poland huko Warsaw siku ya Ijumaa. Siku nne baadaye, Wajerumani watakuwa wenyeji wa Columbia mjini Gelsenkirchen kumaliza msimu wa soka.

Kisha itakuwa na mechi ya marudiano na Japan Septemba 9, ambao waliwashinda katika mechi yao ya ufunguzi ya Kombe la Dunia huko Qatar. Siku tatu baada ya hapo, watamenyana na Ufaransa. Mnamo Oktoba, kikosi cha Flick kitacheza na Marekani huko Hartford, Connecticut.

Ujerumani bado haijaamua ni wapi makao makuu yao yatakuwa kwa EURO 2024. Wakati wa michuano ya EURO 2020 makao yake makuu yalikuwa Herzogenaurach, mji wa Ujerumani karibu na Nuremberg kusini mwa Ujerumani.

Mnamo Novemba, mataifa 21 kati ya 24 yatakayoshiriki EURO 2024 yatabainishwa. Washiriki watatu wa mwisho wataamuliwa katika mchujo wa kuwania kufuzu mwezi Machi 2024. Droo ya hatua ya makundi inatarajiwa kupangwa Desemba 2, huku Ujerumani ikipangwa Kundi A moja kwa moja kama taifa mwenyeji. Michezo mitatu ya hatua ya makundi ya timu ya taifa ya Ujerumani itafanyika Juni 14, 2024 mjini Munich (mchezo wa ufunguzi wa michuano hiyo), Juni 19 mjini Stuttgart na Juni 23 mjini Frankfurt.

 https://p.dw.com/p/4SWq2