Ujerumani haiwezi tena kushirikiana na Niger kijeshi
17 Julai 2024Akizungumza katika mkutano wa pamoja na Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara, Baerbock amesema licha ya ushirikiano kati ya mataifa hayo kuharibika, bado Ujerumani haija sitisha misaada ya kibinadamu kwa sababu watu wa Niger hawahusiki na kile kilichotokea.
Ujerumani mnamo Julai 6 ilitangaza kwamba itamaliza operesheni kwenye kituo chake cha anga nchini Niger na kuwaondoa wanajeshi wake dazeni tatu waliosalia ifikapo Agosti 31.
Baerbock afanya ziara Afrika Magharibi
Niger imekuwa ikiongozwa na utawala wa kijeshi tangu mapinduzi ya Julai 2023 yaliyomuondoa madarakani Rais Mohamed Bazoum, ambaye amekuwa akishikiliwa kama mfungwa tangu wakati huo.
Aidha utawala huo umewapa kisogo washirika wengine wa Magharibi kama vile Ufaransa na Marekani na kuegemea upande wa Urusi.