Ujerumani haioni sababu ya kurejesha uhusiano na Syria
8 Mei 2023Matangazo
Hii ni licha ya nchi hiyo ya Mashariki ya Kati kurejeshwa katika Jumuiya ya Nchi za Kiarabu mwishoni mwa juma lililopita.
Msemaji wa wizara hiyo ameeleza kuwa utawala wa Syria chini ya Rais Bashar al-Assad unaendelea kukanyaga haki za raia wake kila siku, na kuukwamisha mchakato wa kidiplomasia.
Akizungumza mjini Berlin siku ya Jumatatu, msemaji huyo amesisitiza kuwa hakuna mabadiliko yoyote katika hali halisi nchini Syria, ambayo yangeishawishi Ujerumani kushiriki katika ukarabati wa nchi hiyo na kuiondolea vikwazo.
Aidha, kulingana na wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani, mazingira nchini Syria hayakidhi viwango vya wakimbizi kurudi nyumbani kwa heshima ya ubinadamu.