1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uingereza yahofia machafuko zaidi

9 Agosti 2024

Mamlaka nchini Uingereza zinasema zinajiandaa kwa uwezekano wa machafuko zaidi.

https://p.dw.com/p/4jHeC
Nach Bluttat in Southport - Downing Street
Picha: Henry Nicholls/PA Wire/dpa/picture alliance

Hii ni licha ya kuwapongeza wanaharakati wanaopinga ubaguzi na maafisa wa polisi waliokabiliana na wimbi la mashambulizi ya makundi ya siasa kali za mrengo wa kulia.

Waziri Mkuu Keir Starmer amesema baada ya mkutano wa dharura wa serikali yake na vyombo vya usalama, kwamba nchi imo kwenye hali ya tahadhari.

Zaidi ya watu 500 wametiwa nguvuni na wengine kuanza kuhukumiwa vifungo vya aina mbalimbali jela, kufuatia mashambulizi ya kibaguzi kwenye miji kadhaa ya Uingereza. Watu wengine zaidi wanatazamiwa kupandishwa kizimbani leo Ijumaa.

Machafuko yameshuhudiwa pia Ireland ya Kaskazini, ambapo hapo jana uongozi wa huko ulikutana pia na vyombo vya usalama kujadili njia za kutejesha utulivu.

Chanzo cha machafuko ya sasa kinasemekana kuwa ni taarifa za uongo zilizosambazwa na makundi ya siasa kali juu ya mauaji ya wasichana watatu wa Kiingereza, ambayo yalisema yalifanywa na mhamiaji Muislamu.

Ukweli ni kuwa mashambulizi hayo yalifanywa mvulana wa Kiingereza,  Mkristo, mwenye asili ya Rwanda.