SiasaUingereza
Starmer aahidi kufufua uhusiano na Ulaya
18 Julai 2024Matangazo
Ametoa mwito wa ushirikiano ili kuendelea kuisaidia Ukraine na kukabiliana na matatizo yanayolikumba bara Ulaya ikiwemo uhamiaji haramu, mabadiliko ya tabianchi na usalama wa nishati.
Akiufungua mkutano wa jumuiya ya kisiasa ya Ulaya EPC ambapo zaidi ya viongozi 40 wanakutana katika kasri la Blenheim, mahali alikozaliwa waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Winston Churchill, Starmer ameeleza nia ya kurejesha uhusiano kati ya Uingereza na Ulaya baada ya Brexit.
Kiongozi huyo pia amejitenga na utawala wa serikali iliyopita ambayo ilitishia kujiondoa kwenye mkataba wa kimataifa kuhusu haki za binadamu.