Katika makala ya Mwangaza wa Ulaya, Daniel Gakuba anamulika mtikisiko unaoukabili uhusiano kati ya Umoja wa Ulaya na Urusi, kuhusiana na manyanyaso ya serikali ya Urusi dhidi ya mpinzani mkuu wa rais Vladmir Putin, Alexei Navalny, na hatua ya Urusi kuwatimua mabalozi watatu wa Umoja wa Ulaya katika siku ambapo mkuu wa diplomasia wa umoja huo alipofanya ziara mjini Moscow.