Uholanzi, Ubelgiji zajiunga kwenye uchunguzi kuhusu Wayazidi
26 Juni 2023Matangazo
Timu ya pamoja ya uchunguzi, ilianzishwa na Ufaransa na Sweden Oktoba mwaka 2021 na kuungwa mkono na shirika la Eurojust lenye makao yake mjini The Hague, Uholanzi kwa lengo la kuwafungulia mashtaka wafuasi wa itikadi kali kutoka nchi za kigeni, waliowalenga jamii ya Wayazidi wakati wa vita katika nchi za Syria na Iraq.
Tayari tumu hiyo imefanikiwa kuwatambuwa watu wawili raia wa Ufaransa, mtu na mkewe wafuasi wa itikadi kali, waliohusika kwa mauaji ya mtu wa jamii ya Yazidi.
Timu hiyo ya uchunguzi wa pamoja ni sehemu ya juhudi pana za kimataifa za kutafuta haki kuhusu mauaji yaliyowalenga Wayazidi, waliolengwa na kundi linalojiita Dola la Kiislamu.