1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MichezoCosta Rica

Uhispania yaanza vyema Kombe la Dunia la Wanawake

Saumu Njama Selina Mdemu
21 Julai 2023

Michuano ya Kombe la Dunia la Wanawake imeanza vyema kwa wahispania baada ya kuwalaza wapinzani wao Costa Rica mabao 3-0

https://p.dw.com/p/4UEBX
Frauen Fußball WM 2023 | Spanien v Costa Rica
Kombe la Dunia la Wanawake 2023 Uhispania na Costa Rica Picha: Catherine Ivill/Getty Images

Wahispania wameonyesha ni kwa namna gani wao ni miongoni mwa wanaopewa nafasi kubwa katika mechi yao ya kwanza ya kundi C mjini Wellington, kwa kuwafunga 3-0 ndani ya dakika sita tu, wapinzani wao Costa Rica ambao walitumia takribani mchezo mzima kujilinda.

Bao la kwanza lilipatikana pale mlinzi wa Costa Rica Valeria del Campo alipoinasa krosi iliyomsababishia wao kujifunga kutoka kwa Esther Gonzalez. Huku goli la pili likiwekwa wavuni na Aitana Bonmati na bao la tatu likitundikwa na Esther Gonzalez.

Soma Zaidi: Kombe la Dunia la Wanawake laanza kutimua vumbi

Mchezaji wa Barcelona, ​​Aitana Bonmati alikuwa mchezaji wa kiwango cha juu wakati wote wa shindano hilo, huku akitengeneza nafasi nyingi bora za Uhispania kuweza kupata magoli. Bonmati ni mmoja wa wachezaji watatu waliorejea kutoka uhamishoni kwa miezi tisa kucheza Kombe la Dunia.

Mshindi wa Ballon d'Or

Kocha Jorge Vilda alidokeza kuwa mshindi wa tuzo ya Ballon d'Or mara mbili wa Uhispania Alexia Putella atakua miongoni mwa wachezaji wa akiba kutokana na jeraha baya la goti huku Bonmati na Esther wakiendeleza mashambulizi kwenye eneo la hatari la Costa Rica.

Frauen Fußball WM 2023 | Spanien v Costa Rica
Mchezaji wa Uhispania na mchezaji wa Costa Rica. Kombe la Dunia la Wanawake 2023Picha: Catherine Ivill/Getty Images

Kipa wa Costa Rica Daniela Solera, aliokoa mkwaju wa penalti iliyopigwa na Jennifer Hermoso, katika kipindi cha kwanza na akiingia kati mara kadhaa, lakini hiyo haikuwa tija kwa Wahispania ambao walipanda kileleni mwa kundi lao kabla ya mchezo wa Japan dhidi ya Zambia siku ya Jumamosi.

Timu hizo ziliwahi pia kutoka sare ya mabao zilipovaana katika mechi yao ya kwanza yaKombe la Dunia mwaka  2015. Uhispania kwa sasa iko nafasi ya sita katika viwango vya ubora wa wanawake na imeonyesha uwezo wake wa kiufundi kwa kuifunga Costa Rica mara tatu katika dakika sita mfululizo.

 

Tazama: 

 

Chanzo/RTRE