1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhamishajii wa wapiganaji na raia waanza Syria

Admin.WagnerD28 Desemba 2015

Wapiganaji 450 na raia wakiwemo majeruhi wameanza kuhamishwa Jumatatu (28.12.2015) kutoka miji mitatu ya Syria kwa kuzingatia makubaliano ya nadra kati ya serikali na waasi.

https://p.dw.com/p/1HUSj
Hali katika mji uliozingirwa wa Zabadani.
Hali katika mji uliozingirwa wa Zabadani.Picha: picture alliance/abaca

Chini ya makubaliano hayo wapiganaji waasi waliojichimbia kwa miezi kadhaa katika mji huo karibu na mpaka na Lebanone weameahidiwa kupelekwa kwa salama hadi uwanja wa ndege wa Beirut kabla ya baadae kuingizwa Uturuki.

Hapo mwezi wa Septemba pande pande zote mbili zimefikia makubaliano ya kusitisha mapigano kwa miezi sita katika mji wa Zabadani ngome ya mwisho inayoshikiliwa na waasi kwenye mpaka na Lebanone na katika vijiji viwili vya mwisho vinavyoshikiliwa na serikali vya Washia vya Fuaa na Kafraya vilioko katika jimbo la kaskazini magharibi la Idlib.

Makubaliano hayo yaliofikiwa chini ya usimamizi wa Umoja wa Mataifa yanatowa nafasi ya kusitishwa kwa mapigano ili kuwezesha kuingizwa kwa misaada ya kibinaadamu na baadae kuhamishwa kwa raia waliojeruhiwa na wapiganaji.

Wapiganaji wameanza kuondolewa

Kwa mujibu wa Rami Abel Rahman mkuu wa shirika la uangalizi wa haki za binaadamu nchini Syria tayari zaidi ya wapiganaji 120 na raia waliojeruhiwa wameanza kondoka Zabadani.Ameongeza kusema kwamba takriban watu 335 wakiwemo ria wameanza kuondoka Fuaa na Kafraya kurejea kwenye maeneo yanayoshikiliwa na serikali kwa kupitia nchi mbili jirani za Lebanone na Uturuki.

Wanajeshi wa Syria katika mapambanao ya Zabadani.
Wanajeshi wa Syria katika mapambanao ya Zabadani.Picha: picture-alliance/dpa/Sana

Wale waliondolewa kutoka vijiji vya Fuaa na Kafraya watasafirishwa kwenda Uturuki kwa kupitia kituo cha mpakani cha al -Hawa kilioko kati ya Syria na Uturuki kabla ya kusafirishwa kwa ndege kwenda uwanja wa ndege wa Beirut na baadae kwa kutumia barabara kwenda Damascus.

Wale wanaodoka Zabadani watasafiri kwa kuvuka mpaka hadi Lebanone na kwenda kwa ndege huko Beirut na baadae Uturuki kabla ya kurudishwa tena kwenye maeneo yanayosihikiliwa na wapinzani nchini Syria.

Lengo la jumla

Makubaliano hayo ya kuwahamisha maelfu ya wapiganaji wa jihadi na raia kutoka kusini mwa Damascus yalikwama hapo Jumamosi kufuatia kifo cha kiongozi wa waasi Zahran Alloush.

Zahran Alloush kiongozi wa kundi la waasi la Jeshi la Kiislamu nchini Syria aliyeuwawa.
Zahran Alloush kiongozi wa kundi la waasi la Jeshi la Kiislamu nchini Syria aliyeuwawa.Picha: Getty Images/AFP/ABD DOUMANY

Serikali ya Bashar al Assad huko nyuma iliwahi kufikia makubaliano kadhaa ya kusitisha mapigano na makundi ya waasi.

Kwa kawaida makubaliano ya usuluhishi yanayofikiwa ndani ya nchi huwapa nafasi waasi ya kusalimisha silaha zao ili badala yake kuwezeha misaada ya kibinadamu kufikishwa kwa raia wanaoishi kwenye maeneo yaliyozingirwa.

Umoja wa Mataifa na serikali za kigeni zimekuwa zikijaribu kufanikisha usitishaji wa mapigano wa maeneo na kuhamisha wapiganaji na raia kwa usalama kama hatua za kufikia lengo la jumla la kukomesha vita vya wenyewe kwa wenyewe vya takriban miaka mitano nchini Syria.

Mwandishi: Mohamed Dahman /Reurets/AFP

Mhariri: Mohammed Khelef