1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ugiriki kuwafunza marubani wa Ukraine kurusha ndege za F-16

22 Agosti 2023

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema kuwa Ugiriki imejitolea kuwapatia mafunzo marubani wa Ukraine ya kuzirusha ndege za kivita chapa F-16.

https://p.dw.com/p/4VQUA
Ukraine imeukaribisha kwa mikono mwili utayari wa Ugiriki kuwafunza marubani wake kuzirusha ndege chapa F-16.
Ukraine imeukaribisha kwa mikono mwili utayari wa Ugiriki kuwafunza marubani wake kuzirusha ndege chapa F-16. Picha: Lithuanian Ministry of National Defense/AP Photo/picture alliance

Hiyo ni baada ya taifa lake kupata ahadi ya kupokea aina hiyo ya ndege kutoka Denmark na Uholanzi.

Kiongozi huyo ametoa taarifa hiyo baada ya kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Ugiriki Kyriakos Mitsotakis mjini Athens Jumatatu jioni. Zelensky alikwenda Ugiriki kwa ziara fupi kushiriki kikao cha viongozi wakuu wa mataifa ya mashariki mwa Ulaya na kanda ya Balkani.

Amesema Ukraine imeukaribisha kwa mikono mwili utayari wa Ugiriki kuwafunza marubani wake kuzirusha ndege chapa F-16 ambazo serikali mjini Kyiv inatarajia kuanza kuzipokea katika miezi inayokuja.

Jeshi la Anga la Ugiriki kwa sehemu kubwa linatumia aina hiyo ya ndege na marubani wake wanasifika kwa ujuzi mkubwa wa kuzitumia. Mnamo mwishoni mwa juma Ukraine iliahidiwa kupatiwa ndege karibu 60 za aina hiyo kuimarisha anga yake dhidi ya hujuma za Urusi